Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Juni 05, 2023 Local time: 22:26

Matayarisho ya kuapishwa rais wa nne Kenya yamekamilika


Rais mteule Uhuru Kenyata akihutubia taifa baada ya kutangazwa mshindi na Mahakama Kuu
Wananchi wa Kenya, wanasuburi kwa hamu sherehe ya kihistoria ya kumwapisha Rais mteule wa taifa hilo Uhuru Muigai Kenyatta, kukiwa na usalama wa hali ya juu.

Kuna hali ya msisimko na matarajio makubwa, hasa utendaji kazi katika serikali mpya ya Kenya.

Uhuru Kenyatta alishinda kwa zaidi ya kura 700,000 na baada ya mahakama ya juu nchini Kenya kuamua kesi iliyowasilishwa na Bwana Raila Odinga ya kupinga matokeo ya ushindi wa Rais katika uchaguzi mkuu uliofanyika mwanzoni mwa mwezi Machi, Bwana Odinga alikubali uamuzi wa mahakama.

please wait

No media source currently available

0:00 0:04:59 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Hatua hiyo iliondoa wasiwasi kwa watu waliohofia kuwa huwenda Kenya ikakumbwa tena na mgogoro wa kisiasa na ghasia, kama zile zilizotokea mwaka wa 2008. na ikafungua njia kwa rais wa nne kuapishwa kama ilivyohitajika na katiba hapo April 9.
Matayarisho yamekuwa yakifanyika katika uwanja wa michezo wa Kasarani Sports Center.

Wakati huo huo taarifa kutoka serikalini inasema kuwa marais 13 walioalikwa kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais wan ne wa Jamhuri ya Kenya, bwana Uhuru Kenyatta wamethibitisha kuhudhuria.

Rais wa Uganda Yoweri Museveni amepangiwa kutoa hotuba kwa niaba ya marais wengine watakaohuhduria. Haijabainika iwapo Rais Omar Al-Bashir wa Sudan atahudhuria, japokuwa ni miongoni mwa wageni walioalikwa.

Sherehe hiyo ya kitaifa pia itaashiria siku ya mwisho kwa Rais Mwai Kibaki kuwa ofisini kama rais wa Kenya.
XS
SM
MD
LG