Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 16:14

Uhuru aongoza katika kura ya maoni Kenya


Naibu Waziri Mkuu wa Kenya, Uhuru Kenyatta.
Naibu Waziri Mkuu wa Kenya, Uhuru Kenyatta.

Kufuatia ushindi huo wa kisiasa wa kenyatta baadhi ya wanasiasa wamevihama vyama vyao na kujiunga kwenye chama chake cha National Alliance

Kura ya maoni nchini Kenya inaonyesha kuwa Naibu Waziri Mkuu, Uhuru Kenyatta, ana nafasi kubwa zaidi ya kumshinda Waziri Mkuu Raila Odinga kwenye uchaguzi mkuu ujao ikiwa ataungana na Naibu Waziri Mkuu mwingine, Musalia Mudavadi.

Kulingana na maoni ya kura, ni kwamba Kenyatta anashikilia asilimia 50 ya kura wakati bwana Odinga ana asilimia 43. Kura hii ya maoni inafuatia uchaguzi mdogo uliofanyika hivi karibuni katika maeneo matatu ya ubunge pamoja na sehemu kadhaa za udiwani ambapo Kenyatta alimshinda Odinga kwa kuchukua viti viwili vya ubunge huku Odinga akijipatia kiti kimoja tu.

Vile vile Kenyatta alifanikiwa kujipatia viti kadhaa katika nafasi ya udiwani katika sehemu zilizo mbali na ushawishi wake wa kisiasa.

Kufuatia ushindi huo wa kisiasa wa Kenyatta, wanasiasa kadhaa mashuhuri nchini Kenya wameanza kuvihama vyama vyao vya kisiasa na kujiunga na chama cha Kenyatta cha National Alliance.

Kenya inatarajiwa kufanya uchaguzi mkuu mwezi Machi mwakani. Baadhi ya wananchi wanakhofia kutokea tena kwa machafuko ya kisiasa kama yale yaliyotokea katika uchaguzi mkuu uliopita wa mwaka 2008, ambapo watu wasiopungua 1,000 walipoteza maisha na wengi kukoseshwa makazi ndani ya nchi yao.
please wait

No media source currently available

0:00 0:02:28 0:00
Kiungo cha moja kwa moja
XS
SM
MD
LG