Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 04, 2022 Local time: 17:12

Ugiriki na EU waanza kuwapeleka Uturuki wahamiaji wa Ulaya


Ugiriki na Umoja wa Ulaya wameanza kuwaondoa wahamiaji kutoka visiwa vya Lesbos na Chios na kuwapeleka Uturuki kwa mujibu wa makubaliano yalio na utata ya mwezi Machi kati ya Umoja wa Ulaya na Ankara.

Licha ya utabiri wa ghasia, kuondoka kwa meli ya kwanza kutoka Lesbos mapema jumatatu kulitokea bila ghasia yeyote wakati idadi ndogo ya waandanamaji walikusanyika katika bandari kulaani mpango huo.

Maafisa walianza kuondoa mabasi yaliojaa watu kutoka kwenye kambi ya wakimbizi huko Moria nyakati za alfajiri na kuwapeleka bandarini katika mji mkuu wa kisiwa hicho Mytilini ambapo walipandishwa boti ya Uturuki kwa safari fupi kuelekea Uturuki.

XS
SM
MD
LG