Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 13, 2024 Local time: 06:47

Uganda yatafakari kuondoa majeshi yake Sudan Kusini


wanajeshi wa Uganda wakipiga doria katika mji wa Bor, jimbo la Jonglei Sudan Kusini.
wanajeshi wa Uganda wakipiga doria katika mji wa Bor, jimbo la Jonglei Sudan Kusini.
Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Uganda,Sam Kutesa anasema, wanajeshi wa jeshi la Uganda (UPDF) wanaoisaidia serikali ya Juba kupigana na waasi katika nchi jirani ya Sudan Kusini wataanza kuondolewa mwanzoni mwa mwzi wa April.

Uganda imeshinikizwa na baadhi ya nchi za kanda hiyo pamoja na Marekani kuondowa wanajeshi wake kutoka Sudan Kusini. Hata hivyo msemaji wa wizara ya mambo ya nchi za nje Fred Opolot amekanusha kwamba jambo hilo.

Anasema pendekezo la kuwaondowa wanajeshi linafuatia mashauriano na srikali ya Juba na Mamlaka ya Maendeleo ya serikaali za Afrika Mashariki na Pembe mwa afrika (IGAD), pamoja na Umoja wa Afrika, unaopanga kupeleka wanajeshi wengine kusaidia kurudisha hali ya usalama huko Sudan Kusini.
XS
SM
MD
LG