Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Juni 09, 2023 Local time: 10:40

Uganda yapunguziwa misaada kutokana na sheria dhidi ya mashoga


Gazeti la Uganda 'Red Pepper' lililochapisha picha za watu 200 linalodai ni wapenzi wa jinsia moja. Februari 25, 2014

Denmark na Norway zimesema zinapunguza mamilioni ya dola za msaada kwa serikali ya Uganda kutokana na sheria hiyo mpya. Sweden pia imetishia kufanya hivyo.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry amehusisha sheria mpya ya Uganda dhidi ya wapenzi wa jinsia moja na ubaguzi wa rangi katika enzi za Nazi na Afrika Kusini.

Amesema sheria hizo za kupinga wapenzi wa jinsia zimeibua hisia mbalimbali Marekani na kusababisha changamoto kwa sababu haki za mashoga ni haki za kibinadamu.

Denmark na Norway zimesema zinapunguza mamilioni ya dola za msaada kwa serikali ya Uganda kutokana na sheria hiyo mpya. Sweden pia imetishia kufanya hivyo.

Thamani ya shilingi ya Uganda ilishuka kwa zaidi ya asilimia 2 Jumatano, siku mbili baada ya rais wa Uganda Yoweri Museveni kutia saini sheria hiyo yenye adhabu kali kwa wapenzi wa jinsia moja Jumatatu .

Sheria hiyo mpya imepiga marufuku uhamasishaji wa mapenzi ya watu wa jinsia moja na wale wote wanaojihusisha na maswala ya ushoga wanaweza kukabiliwa na adhabu ya kifungo cha maisha jela.
XS
SM
MD
LG