Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 10:43

Uganda yamfukuza mwanasiasa wa upinzani wa Rwanda Robert Mkombozi


Robert Mkombozi, Kiongozi wa chama cha upinzani cha Rwanda National Congress (RNC)
Robert Mkombozi, Kiongozi wa chama cha upinzani cha Rwanda National Congress (RNC)

Uganda imesema imemtimua mmoja wa viongozi wa kundi lililopigwa marufuku la upinzani nchini Rwanda, ikiwa ni ishara zaidi ya kuimarishwa kwa uhusiano kati ya Kampala na Kigali, baada ya miaka mingi ya mvutano.

Kufukuzwa kwa Robert Mukombozi wa Chama kilicho uhamishoni cha Rwanda National Congress (RNC), kumefuatia ahadi ya mtoto wa Rais wa Uganda Yoweri Museveni, Jenerali Muhoozi Kainerugaba, ya kukabiliana na kundi ambalo Kigali inalichukulia kuwa la kigaidi.

Kuwepo katika ardhi ya Uganda kwa watu wanaoshukiwa kuwa waasi wanaotaka kumpindua Rais wa Rwanda Paul Kagame limekuwa donda sugu katika uhusiano kati ya majirani hao wawili.

Kainerugaba alisema kwenye ukurasa wake wa Twitter kwamba Mukombozi alifukuzwa, akimtaja kuwa "adui wa Rwanda na Uganda" na kuweka picha zake akitembea kwelekea kwenye ndege, katika uwanja wa ndege wa Entebbe.

Mukombozi, Mnyarwanda aliyezaliwa Uganda, alifanya kazi kama mwandishi wa habari na vyombo vya habari vya ndani, kabla ya kwenda Rwanda lakini alitofautiana na serikali na amekuwa akiishi uhamishoni nchini Australia, kwa mujibu wa maafisa wa kijasusi wa Uganda.

Mtoto huyo wa Museveni amekuwa na mchango mkubwa katika kurekebisha uhusiano wa muda mrefu wa uhasama na Kigali, ikiwa ni pamoja na kufanya mazungumzo na Kagame ambayo yalipelekea kufunguliwa tena kwa mpaka wa ardhi mwezi Januari baada ya kufungwa kwa miaka mitatu.

RNC ilianzishwa mwaka 2010 na mkuu wa zamani wa jeshi la Rwanda, Kayumba Nyamwasa na mkuu wa zamani wa idara ya ujasusi Patrick Karegeya, ambao wote walikwenda uhamishoni Afrika Kusini na kwendelea kuwa wakosoaji wakali wa Rais Kagame.

XS
SM
MD
LG