Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 04:32

Uganda yajitetea kuingia Sudan Kusini


gari la kijeshi la Uganda likipiga doria katika mji wa Bor, jimbo la Jonglei , Sudan Kusini
gari la kijeshi la Uganda likipiga doria katika mji wa Bor, jimbo la Jonglei , Sudan Kusini
Serikali ya Uganda imesema kupeleka wanajeshi wake Sudan Kusini na kujihusisha na mgogoro unaondelea huko Juba ipo chini ya mkataba kati ya serikali zao mbili.
Siku ya Jumatatu, Rais wa Uganda Yoweri Museveni amesema kuwa baadhi ya wanajeshi wake waliuwawa na kujeruhiwa huko Sudan Kusini.

Msemaji wa Jeshi ya Uganda Lt. kanali Paddy Ankunda amesema Jumanne kua, Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir alitoa mualiko kwa jeshi la Uganda kumsaidia dhidi ya waasi wa aliekuwa naibu wake wa zamani Riek Machar.

Katika kikao maalum kilichofanyika Jumanne wiki hii waziri wa ulinzi wa Uganda Dk. Krispus Kiyonga alielezea Bunge kuwa uamuzi wa Raisi Yoweri Museveni hauku unavunja sheria.

Serikali ya Uganda ilituma majeshi yake Sudan Kusini December tarehe 24 mwaka jana na kwa mujibu wa serikali ilikuwa baada ya ombi ya serikali ya Raisi wa Sudan Kusini Salva Kiir.

Kwa wajibu wa Lt. Kanali Ankunda, Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir alikerwa na viongozi wa kikanda ambao hawakuitikia wito wake. Na jeshi la UPDF ndilo limemsaidia.

Raisi wa Uganda Yoweri Museveni akiwa mjini Luanda Angola wiki iliyopita katika taarifa yake kwa Mkutano wa tano wa Wakuu wa viongozi wa mataifa ya nchi za Maziwa Makuu alibaini kuwa jeshi la UPDF linashiriki katika kupambana na wamepoteza baadhi ya askari.

Bungeni Jumanne wiki hii, spika Bibi Rebbeca Kadaga alitaka camati ya ulinzi lijadili mkataba ambayo waziri wa ulinzi Dactari Chrispus Kiyonga alionyesha akitaka bunge liwa unge mkono katika mapambano sudan kusini.

Mkataba wa ushirikiano wa kijeshi kati ya nchi hizo mbili unaelezea kwamba majeshi ya nchi hizo mbili zitashiorikiana katika masuala ya usalama na kwamba jeshi la Uganda linaweza kufanya kazi Sudan Kusini ikihitajika na kadhalika jeshi la Sudan Kusini linaweza kuingia Uganda kusaidia kukiwa na mzozo.

Wabunge wengine walitaka kujua muda ambayo jeshi ya Uganda litaendelea kubaki huko Sudan Kusini kwajili mkataba hauzungumzi suala hilo.
.
Wabunge wa upande waupinzani walihoji uhalali wa mkataba huo kwa ajili ni Uganda na sio Sudan Kusini iliyotia saini na Sudan Kusini ndio wana athirikia zaidi na vita.
Kwa sasa Kamati itasubiri hadi Jumanne wiki ijao kupata jibu kwa maswali yao.
XS
SM
MD
LG