Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 16, 2024 Local time: 16:34

Uganda yafunga mpaka wake na DRC.


Rais wa Uganda, Yoweri Museveni
Rais wa Uganda, Yoweri Museveni
Uganda imeufunga mpaka wake na Jamhuri ya Demokrasia ya Congo wa Bunagana ulioko kusini magharibi mwa Uganda. Mpaka huu hutumika sana na wafanyabiashara wanaoingia nchini Congo na ndio eneo la kwanza lililotekwa na waasi wa kundi la M23 mwezi wa tano mwaka huu ili waweze kukusanya kodi.

Serikali ya Uganda ilitangaza kufungwa kwa mpaka huu siku ya jumanne tarehe 13.
Kwa mujibu wa msemaji wa jeshi la Uganda Kanali Felix Kulayigye, amri ya kufungwa kwa mpaka wa Bunagana ilitolewa jumatatu na Rais wa Uganda Yoweri Museveni baada ya kuombwa na Rais wa Jamhuri ya Demokrasia ya Congo-DRC, Joseph Kabila aufunge mpaka huo.

Kinshasa imekuwa ikilalamika kuwa baadhi ya watu kutoka Uganda na Rwanda wanautumia mpaka wa Bunagana kuwafadhili waasi wa M23 wanaozozana na serikali ya Rais Kabila.

Kufungwa kwa mpaka huu kunamaanisha waasi wa M23 ambao waliyateka maeneo kadhaa mashariki mwa Congo ikiwemo Bunagana na Rutshuru, hawatakuwa na uwezo wa kupata pesa za kutosha za kufadhili kazi zao za uasi. Hii ni kwa sababu wamekuwa wakitegemea sana pesa za ushuru wanaotoza magari yanayoingia nchini Congo.

Wafanyabiashara wa kutoka Uganda na nchi nyingine za Afrika mashariki wanaosafirisha bidhaa zao nchini Congo nao pia wataathirika kwa sababu wengi wao husafirisha bidhaa kama vile sukari, mafuta ya kupikia na matunda kupitia mpaka wa Bunagana.

Ripoti mpya iliyotolewa jumatatu ya wiki hii na World Wildlife Fund for Nature inasema asilimia 50 ya mbao zinazotoka Congo na kuingia Uganda kupitia mpaka wa
Bunagana zinatozwa kiwango cha chini sana cha ushuru.

Mwezi wa kumi, shirika la habari la Reuters lilichapisha ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyosema Uganda na Rwanda zinawafadhili waasi wa kundi la M23.
XS
SM
MD
LG