Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 22, 2024 Local time: 08:07

Uganda: Watoto 6 kutoka familia moja wameambukizwa Ebola


Daktari akionyesha matokeo ya vipimo vya Ebola katika maabara ya Entebbe, Uganda. Aug 2, 2012
Daktari akionyesha matokeo ya vipimo vya Ebola katika maabara ya Entebbe, Uganda. Aug 2, 2012

Kituo cha kudhibithi magonjwa Afrika kimesema kwamba mlipuko wa virusi vya Ebola nchini Uganda haujafikia kiwango ambacho hakiwezi kudhibitiwa licha ya kuongezeka kwa idadi ya watu wanaombukizwa na kufariki.

Maambukizi ya Ebola yamesambaa na kuripotiwa katika jiji la Kampala.

Kaimu mkurugenzi wa kituo hicho Ahmed Ogwell Ouma, amesema kwamba maambukizi ya ebola nchini Uganda yamedhibitiwa.

Ouma pia amesema kwa sasa ni vigumu kutabiri mwenendo wa maambukizi ya virusi hivyo.

Maambukizi ya Ebola aina ya Sudan, visivyokuwa na chanjo yamekuwa yakisambaa nchini Uganda, tangu mwezi Septemba.

Watu 30 wamefariki kutokana na Ebola kote Uganda, huku maambukizi yakiongezeka na kufikia 109, wakiwemo watoto sita kutoka familia moja ambao wamegunduliwa kuambukizwa leo Alhamisi, katika jiji la Kampala.

XS
SM
MD
LG