Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Oktoba 28, 2020 Local time: 17:54

Wanajeshi wa Uganda wauwawa na kundi la watu wenye hasira


Jeshi la Uganda.

Wanajeshi watatu wa Uganda waliuwawa na kundi la watu walio na hasira kwenye mpaka na DRC jana jumapili baada ya kushutumiwa kuwa ni wahalifu na wakazi wa eneo hilo polisi na maafisa wa eneo hilo wameeleza.

“Wanajeshi wetu watatu wameuwawa na kundi la watu na wachunguzi wataendelea kutafuta chanzo cha kuuwawa kwa askari hao, afisa mmoja Peter Debele aliiambia AFP.

Bunduki tatu zimepatikana katika eneo la tukio na watu 8 wamekamatwa kutokana na kuuwawa kwa askari hao aliongeza.

Debele anasema askari hao waliokuwa na silaha waliunganishwa na kikosi cha Uganda kilichokuwa kinalinda eneo la mpakani la Vurra.

Serikali ya nchi hiyo mapema mwaka huu ilipiga marufuku kwa raia kuvaa sare zozote zinazofanana na za kijeshi, hii ni kutokana na wahalifu wengi kutumia sare kama za kijeshi kufanyia uhalifu.

Facebook Forum

Kura ya Maoni : Uchaguzi Tanzania

Kama unapiga kura leo utampigia nani kura yako ya urais?

Kura hii ya maoni si ya kisayansi na inaonyesha maoni ya waliojibu maswali tu.

Kama unapiga kura leo utampigia nani kura yako ya urais?

Kura hii ya maoni si ya kisayansi na inaonyesha maoni ya waliojibu maswali tu.

XS
SM
MD
LG