Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Julai 17, 2024 Local time: 18:46

Uganda: Vyombo vya habari vyawasilisha shauri mahakamani kupinga sheria mpya kuhusu matumizi ya intaneti


Rais wa Uganda Yoweri Museveni
Rais wa Uganda Yoweri Museveni

Vyombo vya habari vya Uganda pamoja na wanaharakati wa kutetea haki za binadamu Jumatatu wamewasilisha shauri mahakamani kupinga sheria mpya yenye utata kuhusu matumizi ya intaneti, ambayo wanasema inalenga kuzuia uhuru wa kujieleza na kuwanyamanzisha wapinzani.

Jumla ya walalamikajii 13, kikiwemo kituo cha televisheni cha mtandaoni, waliwasilisha shauri hilo katika mahakama ya katiba juu ya sheria hiyo, ambayo ilitiwa saini na kuwa sheria na Rais Yoweri Museveni wiki iliyopita.

Sheria hiyo ya kutumia vibaya intaneti “inatishia uhuru wa kujieleza na inalenga wale ambao wana maoni tofauti na serikali”, moja wa walalamikaji, Norman Tumuhimbise ameliambia shirika la habari la AFP.

Kulingana na ombi hilo, serikali imepewa siku saba kuwasilisha utetezi wake lakini haijulikani lini kesi hiyo itaanza kusikilizwa

XS
SM
MD
LG