Kwa mujibu wa shirika la umoja wa mataifa la kuhudumia Watoto, taifa hilo la Afrika Mashariki ndilo pekee hivi sasa Afrika ambako shule bado zimefungwa.
Kwa mara ya kwanza Uganda ilifunga shule machi 2020, muda mfupi baada ya mlipuko wa kwanza wa virusi vya corona kuthibitishwa kwenye bara la Afrika.
Baadhi ya madarasa yalifunguliwa tena mwezi February lakini yakafungwa mwezi Juni wakati nchi ilipokaibiliwa na ongezeko la maambukizo ya corona.
Masharti haya ya sasa ya kufungwa shule yanatarajiwa kufika hadi mapema mwaka 2022.
“Kubaki nyumbani mara nyingine huwezi kuwa na ari ya kusoma vitabu na unaweza kufanya hivyo kidogo, mara nyingine ukasahau ulichofundishwa shule. Kwa hiyo unaacha hata kusoma vitabu kwa sababu wamekuwa wakituambia tunarejea shule, tunarejea shule. Unasubiri hadi unachoka na huwezi hata kusoma kitabu,” alisema mwanafunzi mmoja aliye nyumbani.
Hadi sasa Uganda imefikia nusu ya utoaji wa chanjo dozi milioni 2.5 ya covid 19 kukiwa na watu laki saba waliopatiwa chanjo kamili.
Baadhi ya raia wa Uganda wanasema serikali haijapata njia yenye mafanikio ya kuwawezesha wanafunzi kuendelea na masomo wakati huu ambapo shule zimefungwa.