Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 22:47

Uganda kuwaadhibu vikali wakeketaji wanawake


Nighti Aparo akisimama nje ya nyumbani kwao kaskazini mwa Uganda.
Nighti Aparo akisimama nje ya nyumbani kwao kaskazini mwa Uganda.

Umoja wa mataifa umekuwa ukipinga kukeketwa kwa wanawake ukisema ukeketaji ni udhalilishaji na uvunnjaji wa haki za wanawake na ni zoezi ambalo linahatarisha maisha ya wanawake pia.

Februari sita ni siku ya kimaitaifa ya kupinga ukeketaji wa wanawake. Huku ulimwengu ukisherehekea siku hii, wanaharakati wanaopinga ukeketaji wanalenga kuzishirikisha jamii kukomesha ukeketaji kupitia mazungumzo na kukubali kuwa madhara yanayoletwa na ukeketaji ni mengi na hakuna mazuri yoyote yanayoletwa na utamaduni huu.

Umoja wa mataifa umekuwa ukipinga kukeketwa kwa wanawake ukisema ukeketaji ni udhalilishaji na uvunnjaji wa haki za wanawake na ni zoezi ambalo linahatarisha maisha ya wanawake pia.



Nchini Uganda ni asili mia moja tu ya wanawake ndio wamekeketwa. Jamii zinazowakeketa wanawake hupatikana kaskazini na mashariki mwa Uganda. Jamii hizi ni kama vile Kalenjin, Wapokot, Tepeth na Kadama.

Jamii hizi uona ukeketaji kama kitendo kinachomletea mwanamke hadhi kubwa sana.
Wanawake hukeketwa ili kupunguza tamaa ya kushiriki kwenye kitendo cha ngono kabla ya kuolewa.

Wanawake wamekuwa wakikubali kukeketwa bila pingamizi kwa sababu ni utamaduni waliourithi na ni utaratibu ambao wanafaa kupitia ikiwa watakuwa wanawake wanaoheshimiwa na jamii.

Mwaka wa 2009, bunge lilipitisha mswada kukomesha ukeketaji. Waziri wa jinsia na utamaduni Rukia Nakadama ameeleza adhabu za kisheria kwa wanaokeketa au kukeketwa.

Amesema ukiwa na nia ya kukeketa au ukimkeketa mwanamke unapata kifungo kisichozidi miaka kumi. Ukimkeketa mtu na umwambukize ugonjwa wowote ule, afariki au apate kulemaa, unapata kifungo cha maisha, ikiwa mzazi, mume au mtu mwingine atampeleka au kumlazimisha mwanamke kukeketwa, anapata kifugo cha miaka mitano.

Mkurugenzi wa mfuko wa umoja wa mataifa wa idadi ya watu UNFPA nchini Uganda Janet Jackson anasema ni jukumu la kila mtu kuhakikisha kuwa ukatili dhidi ya wanawake unakomeshwa na umuhimu wa mwanamke kupimwa.

XS
SM
MD
LG