Waziri wa Nishati Ruth Nankabirwa Ssentamu alisema katika taarifa yake akifafanua maendeleo katika sekta hiyo kwamba duru ijayo ya utoaji leseni itatangazwa katika mkutano wa kikanda wa mafuta ya petroli utakaofanyika katika mji mkuu wa Uganda Kampala mwezi Mei.
Hakusema ni vitalu vingapi vitapigwa mnada.
Nchi hiyo ya Afrika Mashariki iligundua akiba ya hidrokabon za kibiashara karibu na mpaka wake wa magharibi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo mwaka 2006. Uzalishaji unatarajiwa kuanza mwaka 2025.
Uganda pia inajenga bomba la kusafirisha mafuta ghafi na kiwanda cha kusafisha mafuta ghafi cha ndani ambacho kitasaidia kufanya rasilimali za mafuta nchini humo kuwa za kibiashara.