Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Machi 02, 2024 Local time: 00:02

Museveni atoa amri kusimamisha uchunguzi wa mauaji ya Kasese


Gari la polis wa Uganda lililochomwa huko Kasese magharibi mwa nchi
Gari la polis wa Uganda lililochomwa huko Kasese magharibi mwa nchi

Rais wa Uganda Yoweri Museveni ametoa amri kusitishwa uchunguzi unaofanywa na kamati ya bunge juu ya mashambulizi yanayodaiwa kutekelezwa na jeshi dhidi ya Ufalme wa Rwenzururu yaliyopelekea vifo vya watu 100.

Museveni alitoa kauli hiyo baada ya kukutana na mkuu wa majeshi, wawakilishi wa polisi, viongozi wa wilaya ya Kasese na viongozi wa ufalme wa Rwenzururu Jumapili.

Hii ni baada ya kamati hiyo kumhoji katika ikulu ya rais ya Entebbe, wakitaka ufafanuzi juu wa yale yaliyojiri na kupelekea vifo vya watu zaidi ya 100.

Wanajeshi na polisi walivamia makao makuu ya mfalme wa Rwenzururu mwanzoni mwa mwezi Disemba.

Mmoja wa wajumbe wa kamati ya bunge inayochunguza mauaji ya Kasese, Muhammad Kivumbi ameiambia Sauti ya Amerika kwamba rais Museveni amesimamisha uchunguzi huo hadi hapo mahakama itakapomaliza kusikiliza kesi inayomkabili mfalme wa Rwenzururu, Charles Wesley Mumbere.

“Rais alifanya mkutano na spika wa bunge na wakakubaliana kuwa kamati ya bunge inayochunguza mauaji ya Kasese isitishe kazi yake mara moja na kuiachia mahakama kufanya maamuzi,” alisema mbunge huyo.

“Hatuna imani kama tutarejea kufanya uchunguzi kwa sababu suala hili lipo mahakamani na linaweza kuchukua karne nzima kuamuliwa,” aliongeza.

Msemaji wa bunge la Uganda, Chris Obore amesema hata hivyo karani wa bunge hajapokea amri yoyote kutoka kwa Museveni, lakini wangali wanaisubiri.

Kwa upande wa uongozi wa Kasese wao wameeleza kuwa na hali ya wasiwasi na kutaka wanajeshi kuondolewa katika eneo hilo kwani kuwepo kwao kumeongeza hali ya wasiwasi.

Winnie Kiiza ambaye ni kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni na pia ni mbunge wa Kasese ameiambia VOA kuwa: “ Watu hawawezi kujihisi wako katika amani na kuwa na imani na serikali iwapo wataona idadi kubwa ya wanajeshi wenye silaha kati yao.”

Aliongeza : “Sasa wanajeshi hao wana wakamata watu kiholela, wanafikia mahali pa kumkamata kila mtu, hili litazua wasiwasi na halitasaidia.”

Wakati huo huo msemaji wa jeshi la Uganda, Paddy Ankunda amekanusha madai ya kuwa vyombo vya usalama na jeshi vimekuwa vikitoa vitisho kwa wananchi wa Kasese.

“Viongozi wametusaliti na hawajatusaidia katika hali hiyo inayoendelea Kasese,” aliiambia VOA kufuatia tuhuma kwamba yeye ndiye aliyekuwa anatoa vitisho.

Alitoa wito kwa viongozi hao wawahamasisha watu na kuwaonyesha njia nzuri badala ya kuilaumu serikali. “Serikali sio tatizo, serikali inajaribu kuhakikisha watu hawa wanapata msaada.

XS
SM
MD
LG