Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Aprili 30, 2025 Local time: 09:17

Uganda imemkamata mkuu wa ADF aliyehusishwa na mashambulizi ya mauaji


Bendera ya Uganda
Bendera ya Uganda

Jeshi lilitangaza Alhamisi kwamba lilimkamata mkuu wa kikosi cha wanamgambo wanaodhaniwa ni Allied Democratic Forces (ADF) katika operesheni iliyowauwa wapiganaji sita wengine

Uganda ilisema Ijumaa kwamba kamanda aliyekamatwa wa kikosi cha wanamgambo wanaotuhumiwa kuwaua watalii wawili wa kigeni mwezi uliopita pia aliongoza mauaji ya kikatili katika shule moja mwezi Juni na kusababisha darzeni ya vifo.

Jeshi lilitangaza Alhamisi kwamba lilimkamata mkuu wa kikosi cha wanamgambo wanaodhaniwa ni Allied Democratic Forces (ADF) katika operesheni iliyowauwa wapiganaji sita wengine.

Uganda inalilaumu kundi la ADF ambalo lina uhusiano na kundi la Islamic State kwa matukio yote ya mauaji ya watalii waliokuwa wakienda kwenye fungate wakiwa na muongozaji wa safari hiyo hapo mwezi Oktoba pamoja na shambulio la shule lililopelekea vifo vya watu 42, wengi wao wanafunzi.

Waathirika walishambuliwa, walipigwa risasi na kuchomwa moto katika uvamizi uliofanyika usiku wa manane kwenye shule ya Mpondwe iliyo karibu na mpaka wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo katika shambulizi baya sana la aina yake kuwahi kutokea nchini Uganda tangu mwaka 2010.

Kundi la ADF ndio lililofanya mashambulizi zaidi ya mauaji ya darzeni ya watu miongoni mwa makundi yenye silaha ambayo yanatatiza hali ya usalama mashariki mwa Congo yaliyoshutumiwa kuwachinja maelfu ya raia katika eneo pamoja na kufanya mashambulizi ya kukatisha mpaka.

Forum

XS
SM
MD
LG