Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Aprili 14, 2024 Local time: 22:55

Uganda yalenga kutokomeza ukimwi


Daktari akitoa damu kupima HIV
Daktari akitoa damu kupima HIV

Na Kennes Bwire, Kampala

Uganda ina matumanini ya kuhakikisha kwamba hakuna maambukizi mapya ya ugonjwa wa ukimwi ifikapo mwaka wa 2030.Kwa sasa, maambukizi yamepungua kutoka watu 180,000 mwaka 1985 hadi watu 99 kila mwaka.

Uganda yalenga kutokomeza ukimwi
please wait

No media source currently available

0:00 0:03:26 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Hata hivyo, shirika linalopambana na maambukizi ya ukimwi nchini humo linaeleza kwamba vita dhidi ya ukimwi vinatatizwa na hali ya vita kutoogopa ugonjwa huo kwa fikra kwamba kuna dawa za kupunguza makali ya ukimwi ARV.

Uganda ilikuwa nchi ya kwanza Afrika Mashariki kugundua hali ya ugonjwa wa ukimwi mwaka 1985. Tangu hapo Uganda imepiga hatua kubwa katika kupunguza viwango vya ugonjwa huo na maambukizi kufuatia kampeni ya nguvu iliyoendeshwa na serikali ya nchi hiyo, ikiungwa mkono na mashirika ya kimataifa.

Hivi sasa nchi hiyo, kwa msaada kutoka serikali ya Marekani, ina matumaini makubwa ya kutokomeza kabisa maambukizi ifikapo mwaka 2030 kwa kupitia program mbali mbali zinazoendeshwa nchini humo ikiwa ni pamoja na upatikanaji madawa na mbinu endelevu za kinga.

XS
SM
MD
LG