Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 16, 2024 Local time: 11:27

Ufilipino yaongeza umri wa ridhaa ya kufanya mapenzi


Ramani wa mji wa Ufilipino wa Mindanau
Ramani wa mji wa Ufilipino wa Mindanau

Ufilipino imeongeza umri wa ridhaa ya kufanya mapenzi hadi miaka 16 baada ya kurekebisha sheria iliyodumu karibu karne nzima.

Wanaharakati wa haki za watoto wamesema Jumatatu kwamba hatua hiyo itasaidia kuwalinda watoto dhidi ya ubakaji na unyanyasaji.

Taifa hilo lenye waumini wengi wa dini ya Katoliki ni moja ya nchi za dunia yenye sheria ya umri mdogo sana wa ridhaa ya kufanya mapenzi, ikiruhusu watu wazima kufanya mapenzi na watoto wenye umri wa miaka 12 iwapo wataridhia.

Chini ya sheria iliyofanyiwa marekebisho na kusainiwa na rais Rodrigo Duterte siku ya Ijumaa na kuwekwa hadharani leo Jumatatu, kufanya mapenzi na mtu aliye chini ya umri wa miaka 16 itakuwa kinyume cha sheria na kutakuwa na adhabu ya kifungo cha hadi miaka 40 jela.

Ruhusa itatolewa kwa wanandoa vijana ili mradi tofauti ya umri kati yao isizidi miaka mitatu na tendo la mapenzi liwe la maelewano.

XS
SM
MD
LG