Ufaransa imeikosoa NATO kwa kushindwa kulinda raia nchini Libya.
Hayo yamesemwa na waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa Alain Juppe wakati akizungumza na radio ya Ufaransa na kusema kuwa NATO ni lazima itoe mchango mkubwa kuangamiza silaha nzito za Moammar Gadhafi.
Juppe amesema atazungumzia suala hilo katika mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa umoja wa ulaya leo na ule wa mawaziri wa NATO wiki ijayo.
Ndege za NATO zilianza mashambulizi mwezi uliopita baada ya umoja wa mataifa kupitisha azimio la marufuku ya kurusha ndege katika anga ya Libya katika juhudi za kulinda raia dhidi ya mashambulizi ya bwana Gadhafi.
Licha mashambulizi ya anga mapigano bado yanaendelea baina ya waasi na vikosi vya usalama vya bwana Gadhafi.
Jumatatu uongozi wa mpito wa waasi ulikataa pendekezo la sitisho la mapigano lililotoklewa na umoja wa ulaya.
Ufaransa yaishutumu NATO kushindwa kulinda raia wa Libya

waziri wa mambo ya nje wa ufaransa amesema NATO imeshindwa kulinda raia wa Libya