Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Februari 08, 2023 Local time: 05:53

Ufaransa yaingia robo fainali baada ya kuitoa Poland  


Olivier Giroud na mwenzake Kylian Mbappe wakisherehekea bao la kwanza la Ufaransa kwenye Kombe la Dunia Qatar.

Timu ya taifa ya Ufaransa Le Bleu imekata tiketi ya kuingia  robo fainali ya michuano ya kombe la dunia baada ya kuifunga Poland bao 3-1 katika uwanja wa   Al Thumama.

Giroud alifunga bao lake la 52 la Ufaransa na kuvuka rekodi ya Thierry Henry kwa kumaliza kipindi cha kwanza na kusaidia Les Bleus kutinga hatua ya 16 bora mjini Doha na sasa kutinga robo fainali dhidi ya England au Senegal.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 36, ambaye alikuwa amefikisha idadi ya Henry ya 51 baada ya kufunga mara mbili katika ushindi wao wa ufunguzi wa Kundi D dhidi ya Australia, alivunja rekodi katika mechi yake ya 117 akiwa na Ufaransa.

Kylian Mbappe akipachika goli la 3 la Ufaransa kuishinda Poland katika Kombe la Dunia Qatar
Kylian Mbappe akipachika goli la 3 la Ufaransa kuishinda Poland katika Kombe la Dunia Qatar

Mshambuliaji hatari wa Ufaransa Kylian Mbappe aliifungia Ufaransa bao la pili dakika ya 74 kabla ya kufunga bao la pili dakika za lala salama na kutengeneza jumla ya mabao matano mawili zaidi ya mchezaji yeyote kwenye michuano hiyo.

Mshambuliaji wa Poland Robert Lewandowski alipachika bao kwa njia ya penati iliyopigwa kwa mara ya pili katika dakika ya 99 na kuongeza faraja kwa Poland ma kumnyima Hugo Lloris kumaliza mechi bila kufungwa bao katika mechi yake ya 142 kwa Ufaransa.

Sasa Ufaransa anamngoja mshindi kati ya Uingereza na Senegal kupambana nae katika robo fainali.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG