Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Juni 24, 2026 Local time: 22:27

Ufaransa, Ujerumani na Uingereza zalaani hatua za Iran kupanua mpango wa nyuklia

Nembo ya Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) ikionyeshwa katika makao makuu ya shirika hilo siku ya ufunguzi wa mkutano wa robo mwaka wa Bodi yake ya Magavana ya mataifa 35 mjini Vienna, Austria, Juni 3, 2024. REUTERS.

Ufaransa, Ujerumani na Uingereza Jumamosi zililaani hatua za hivi karibuni za Iran, kama ilivyoripotiwa na IAEA, ili  kupanua zaidi mpango wake wa nyuklia.

Iran imepiga hatua zaidi katika kwenye kinyume na makubaliano ya JCPoA, kwa kuendesha mitambo mingi ya ziada katika eneo la usindikaji la Natanz na kutangaza kuwa itaweka maelfu zaidi ya mabomba katika maeneo yake ya Fordow na Natanz, taarifa hiyo ya pamoja ilisema. Mpango Kamili wa pamoja wa Utekelezaji uliotiwa saini na Iran mwaka 2015.

Uamuzi huu ni kuongezeka zaidi kwa mpango wa nyuklia wa Iran, ambao una hatari kubwa ya kuenea, ilibainisha.

Taarifa ya pamoja ilisisitiza kuwa uamuzi wa Iran wa kuongeza kwa kiasi kikubwa uwezo wake wa uzalishaji katika kituo cha chini ya ardhi cha Fordow ni jambo la kutia wasi wasi.

This item is part of

Forum

XS
SM
MD
LG