Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Septemba 24, 2022 Local time: 23:44

Ufaransa kusaidia pembe ya Afrika tani 400 za chakula


Mwanamke aliyekoseshwa makazi Somalia akiwa amembeba mtoto wake wakisubiri msaada wa chakula

Wataalamu wameonya kuwa uzalishaji wa chakula kusini mwa Somalia bado ni ndogo na kwamba hali ya ukame kote katika eneo inaweza kuendelea na kusambaa.

Meli iliyobeba karibu tani 400 za chakula kwa ajili ya waathiriwa wa janga la ukame na njaa katika pembe ya Afrika inatarajiwa kuondoka ufaransa alhamisi.

Shirika la umoja wa mataifa la chakula –WFP, limesema meli hiyo ya ufaransa imebeba unga wa kutosha , sukari, mchele na mafuta kulisha zaidi ya watu elfu 22 kwa mwezi mmoja.

Chakula hilo kilitolewa kwa ushirikiano wa wafanyabishara wa ufaransa na jumuiya na kitatumika kwa ajili ya operesheni za WFP nchini Somalia . Maafisa wanasema chakula hicho kitawasili baada ya siku 12.

Jumanne Umoja wa mataifa ilisema watu wachache Somalia wanatoroka nyumba zao. Ofisi ya umoja wa mataifa kwa ajili ya masuala ya kibinadamu imesema watu elfu tano wamehamia Mogadishu mwezi huu ukilinganisha na mwezi Julai walikuwa watu elfu 28.

Ripoti ya shirika hilo ya wiki imesema idadi ya wasomali wanaokwenda kwenye makambi ya wakimbizi ya Kenya na Ethiopia pia imepungua.

Wataalamu wameonya kuwa uzalishaji wa chakula kusini mwa Somalia bado ni ndogo na kwamba hali ya ukame kote katika eneo inaweza kuendelea na kusambaa.

Umoja wa mataifa tayari ilitangaza ukame katika maeneo matano kusini mwa Somalia.

XS
SM
MD
LG