Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 26, 2024 Local time: 09:17

Ufaransa kupiga kura Jumapili kwa duru ya mwisho ya upigaji kura wa rais


Maafisa wa uchaguzi wakiondoa kisanduku cha kura kuhesabu kura za duru ya pili ya uchaguzi wa rais wa Ufaransa wa mwaka 2012 huko Illkirch-Graffenstaden karibu na Strasbourg, May 6, 2012. (Reuters)
Maafisa wa uchaguzi wakiondoa kisanduku cha kura kuhesabu kura za duru ya pili ya uchaguzi wa rais wa Ufaransa wa mwaka 2012 huko Illkirch-Graffenstaden karibu na Strasbourg, May 6, 2012. (Reuters)

Ufaransa itapiga kura Jumapili kwa duru ya mwisho ya upigaji kura katika uchaguzi wa rais, huku Marine Le Pen wa chama cha siasa kali za mrengo wa kulia cha National Rally akiwa pointi chache tu nyuma ya Emmanuel Macron

Ufaransa itapiga kura Jumapili kwa duru ya mwisho ya upigaji kura katika uchaguzi wa rais, huku Marine Le Pen wa chama cha siasa kali za mrengo wa kulia cha National Rally akiwa pointi chache tu nyuma ya Emmanuel Macron aliyeko madarakani. Ushindi wa Le Pen utakuwa na athari kubwa kwa usalama wa Ulaya kufuatia uvamizi wa Russia dhidi ya Ukraine.

Katika mjadala mkali wa televisheni Jumatano, Rais aliye madarakani Emmanuel Macron alitaka kuangazia uhusiano kati ya chama cha mrengo wa kulia cha Marine Le Pen na Rais wa Russia Vladimir Putin. Chama chake cha Kitaifa cha Rally kilichukua mikopo kadhaa kutoka Russia mnamo mwaka 2014, ikijumuisha mkopo wa dola 9.75 milioni kutoka Benki yenye mahusiano na Kremlin First Czech Russian Bank.

XS
SM
MD
LG