Ufaransa inahofia uhusiano mbaya na Mali usije kurudia na nchi ya Burkina Faso yenye utawala wa kijeshi, ambako makundi mengine katika ushirikiano wake wa kijeshi dhidi ya wanajihadi wa Afrika Magharibi yanaweza kuanguka.
Wanajeshi wa Ufaransa waliondoka Mali mwaka jana, baada ya mapinduzi ya mwaka 2020 katika lililokuwa koloni la zamani la Ufaransa kushuhudia watawala wake wakiwa karibu na Russia.
Burkina Faso pia wakati mmoja iliwahi kuwa chini ya utawala wa Ufaransa sasa inaonekana kusonga mbele katika njia hiyo hiyo baada ya maafisa kuchukua madaraka huko mwezi Septemba katika mapinduzi ya pili miezi minane iliyopita.
Ufaransa ina vikosi maalum 400 vilivyoko nchini humo ili kupambana na uasi wa wanajihadi.
Lakini uhusiano umedorora katika miezi ya karibuni, na Waziri Mkuu wa Burkina Faso, Apollinaire Kyelem de Tembela mwezi Novemba alisema anatumai “kutofautisha mahusiano yao ya kiushirika" katika vita dhidi ya wanajihadi.
"Russia ni chaguo la busara," Tembela alisema Jumamosi baada ya kukutana na balozi wa Russia, Alexey Saltykov.
Waziri Mkuu pia alifanya ziara ya kimkakati huko Moscow mapema Desemba.
Nchini Mali, Ufaransa ilikosa upendeleuhsiano wao uliingia dosari na utawala wa kijeshi baada ya madai ya kuwasili mwaka 2021 kwa mamluki wa kundi la Russia la Wagner ili kuimarisha vikosi vya serikali.