Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Juni 14, 2024 Local time: 19:19

Euro 2016: Ronaldo na Ureno wajikongoja kuelekea nusu fainali


UEFA EURO 2016
UEFA EURO 2016

Katika mechi kali na ya kusisimua iliyochezwa jana kati ya Ureno na Poland, Ureno wamefanikiwa kuingia nusu fainali ya michuano ya UEFA EURO 2016 kwa mikwaju ya penati huku mchezaji bora wa Ureno Cristiano Ronaldo akionekana kupwaya katika mechi hiyo.

Nyota anayechipukia wa Ureno Renato Sanchez alionyesha kiwango cha juu sana kama kiungo wa katikati na wengi kushangazwa na uchezaji mahiri wa mwanasoka huyo mdogo kabisa wa miaka 18.

UEFA EURO 2016
UEFA EURO 2016

​Mchezo huo ulianza kwa matumaini makubwa sana kwa timu ya Poland ambapo nyota wake aneyechezea klabu ya Bayern Munich ya ujerumani Lewandoski aliwapeleka mbele kwa bao lake safi mapema kabisa lakini Ureno walisawazisha bao hilo kupitia kwa nyota mdogo Renato Sanchez.

Poland hawakuonyesha juhudi kubwa sana katika kipindi cha pili haswa baada ya washambuliaji wake Lewandoski na Arkadiusz Milk kuwa kimya katika dakika nyingi sana za kipindi cha pili.

Mechi hiyo iliamuliwa kwa mikwaju ya penati ambapo matokeo yalikuwa magoli 5 kwa Ureno na magoli 3 ya Poland.

Ureno sasa watakabiliana na mshindi wa leo kati ya Wales na Ubelgiji katika hatua ya nusu fainali.

XS
SM
MD
LG