Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Machi 23, 2025 Local time: 23:19

Uchunguzi waanzishwa kufuatia ajali ya ndege ya Japan


Mabaki ya ndege ya abiria ya Japan iliyochomeka baada ya ajali kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Haneda, Tokyo on January 3, 2024.
Mabaki ya ndege ya abiria ya Japan iliyochomeka baada ya ajali kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Haneda, Tokyo on January 3, 2024.

Mamlaka zimeanza uchunguzi rasmi wa kilichopelekea ajali ya Jumanne usiku kati ya ndege ya abiria ya Japan na ile ya walinzi wa pwani kwenye njia ya ya  ndege katika uwanja wa Haneda mjini Tokyo, ambapo walinzi watano wa pwani  walikufa.

Ndege hiyo ya abiria ya shirila la ndege la Japan aina ya Airbus A-350 ilikuwa imetua muda sio mrefu kwenye kisiwa cha kaskazini mwa Japan cha Hokkaido, ikiwa na abiria 379 pamoja na wafanyakazi wake.

Video iliyotolewa ilionyesha moto mkubwa ukitokea upande mmoja wa ndege hiyo wakati ilipokuwa ikisafiri kwenye njia ya ndege. Moto huo uliongezeka pale ilipokaribia kusimama huku wafanyakazi wa zima moto wakikabiliana na moto huo. Abiria wote waliokuwa ndani waliweza kutoka salama kwa kutumia milango ya dharura, kabla ya ndege hiyo kuteketea kabisa.

Kwa upande mwingine, rubani wa ndege ya walinda bahari iliyotengenezwa na kampuni ya Havilland ya Canada, na iliyogongana na ile ya abiria, ndiye pekee aliyenusurika kwenye ajali hiyo. Uchunguzi ukiongozwa na idara ya polisi ya Tokyo pamoja na bodi ya Uslama wa safari za ndege Japan, kuhusiana na ajali hiyo tayari umeanza.

Forum

XS
SM
MD
LG