Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Februari 23, 2024 Local time: 12:14

Mahakama Kuu ya Brazil yaombwa ianzishe uchunguzi dhidi ya Rais


Rais wa Brazil, Dilma Rousseff.
Rais wa Brazil, Dilma Rousseff.

Vyombo vya habari vya Brazil vimeripoti kuwa mwendesha mashitaka mkuu nchini humo ameiomba mahakama kuu kuanzisha uchunguzi wa shutuma kuwa Rais Dilma Rousseff anahujumu haki.

Maafisa hawajadhibitisha ripoti hizo zilizojitokeza Jumanne jioni kupitia gazeti la Globo zikidai kwamba Rousseff anashukiwa kuingilia kati uchunguzi unaoendelea dhidi ya kampuni ya mafuta ya Petrobas inayomilikiwa na Serikali.

Magazeti yamemnukuu mwendesha mashitaka Rodrigo Janot akisema kuwa ameomba mamlaka kuchunguza Rousseff pamoja na mtangulizi wake na mshirika wa karibu Luiz Inacio Lula da Silva hasa kufuatia mawasiliano ya simu kati yao wawili.

Rais Rousseff tayari anakabiliwa na uchunguzi unaoweza kupelekea kupigiwa kura ya kutokuwa na Imani naye katika kipindi cha wiki moja.

XS
SM
MD
LG