Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Juni 13, 2024 Local time: 22:58

Meli yatambua chombo cha mawasiliano cha EgyptAir


Maafisa wa usafiri wa anga wa Misri wamesema leo Jumatano kua meli moja ya Ufaransa imenasa sauti kutoka chombo cha mawasiliano ya usafiri wa ndege, kijulikanacho kama Black Box cha ndege ya EgyptAir ambayo ilianguka katika bahari ya Mediteranean mwezi uliopita.

Ajali hiyo iliyotokea Mei 19 iliuwa abiria wote 66 kwenye ndege hiyo. Maafisa wanataka kupata habari kutoka chombo hicho kinachorikodi habari za safari ya ndege ili kuwasaidia kuweza kufahamu kilichosababisha ndege hiyo kuanguka ilipokuwa inakaribia kumaliza safari yake kutoka Paris hadi Cairo.

Wachunguzi wansema moshi ulitokea ndani ya ndege hiyo muda mfupi kabla ya kuanguka, lakini hakukuwa na ishara ya kitu gani kimesababisha moshi huo.

XS
SM
MD
LG