Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Aprili 24, 2024 Local time: 00:51

Umoja wa Mataifa wabashiri kuimarika kwa uchumi duniani


Mkulima wa India akiwa ameshikilia jozi tayari kuwaonesha wanunuzi wa jumla jumla
Mkulima wa India akiwa ameshikilia jozi tayari kuwaonesha wanunuzi wa jumla jumla
please wait

No media source currently available

0:00 0:02:38 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Umoja wa Mataifa unabashiria kuimarika kidogo kwa ukuwaji wa uchumi duniani katika kipindi cha miaka 2 ijayo, kufwatia matokeo ya mwaka jana ambayo hayakuridhisha. Kwenye mkutano mjini Geneva, ambapo kulizinduliwa ripoti ya hali ya uchumi wa dunia na matarajiyo kwa mwaka wa 2016. Ripoti hiyo ilitolewa kwa ushirikiano na mkutano wa umoja mataifa juu ya biashara na maendeleo na kamisheni ya uchumi ya umoja wa mataifa nkwa ajili ya ulaya.

Uchumi wa dunia ulikuwa kwa aslimia 2.4 mwaka 2015. Wachumi wa Umoja wa Mataifa walisema wanatarajia maendeleo kidogo zaidi kwa hali hiyo katika kipindi cha miaka miwili ijayo ambapo ukuwaji wa dunia unaweza kufika asilimia 3.2 ifikapo mwishoni mwa mwaka ujao.

Ripoti hiyo ya pamoja ya Umoja wa Mataifa inabashiri kuendelea kwa ukuwaji katika uchumi wa nchi zilizoendelea kwa kupata kasi mwaka huu na kuvuka asilimia 2 kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2010. Inaeleza kwamba uchumi wa nchi zinazoendelea na zile zinazoinukia unatarajiwa kufanya vizuri zaidi na kuwa na viwango vya ukuwaji kufikia aslimia 4.3 mwaka huu na aslimia 4.8 mwaka 2017.

Ripoti kuhusu ukuaji wa uchumi duniani
Ripoti kuhusu ukuaji wa uchumi duniani

Aidha ripoti inaeleza Asia mashariki na kusini itabaki maeneo yanayokuwa haraka zaidi duniani, licha ya uchumi wa China kupunguka kasi. Mchumi mkuu katika mkutano wa Umoja wa Mataifa juu ya biashara na maendeleo, Alfredo Calcagno alisema China inaendelea kuchangia kwa kiasi kikubwa kwa ukuwaji wa uchumi duniani, licha ya uchumi wake kudorora

Mchumi huyo anaiambia VOA kuwa anaamini dunia inachukulia kwa wasi wasi mkubwa zaidi kuliko inavyostahiki kushuka kwa ukuwaji wa uchumi wa China.

Alisema, kile tunachoshuhudia ni jambo la kawaida, na linahitajika kwa vile viwango vipya na mifumo mipya ya ukuwaji upo endelevu zaidi, kwa sababu inapunguwa hadi aslimia 6.9., huo sio ukuwaji wa polepole. Ni ukuwaji muhimu wa kutosha ili kuweka kichocheo cha ukuwaji wa uchumi duniani.

Mkulima akihesabu mayai ambayo ni chanzo cha uchumi kwa maisha yake.
Mkulima akihesabu mayai ambayo ni chanzo cha uchumi kwa maisha yake.

Calcagno alisema China inaendelea kuwa mojawapo ya kiini cha maendeleo ya uchumi duniani na kwa muda mwingi unaokuja.

Wachambuzi wa Umoja wa Mataifa wanaonya kuwa hatari za siasa za kikanda zinaweza kuwa na athari mbaya kwa imani ya biashara na kuharibu biashara katika kanda ya Ulaya. Wanasema mivutano ambayo haijatatuliwa huko Ukraine, na uhusiano wa kiuchumi unaodorora na Russia, kadhalika mizozo huko Mashariki ya kati ambayo imebuni mzozo wa uhamiaji huko Ulaya, inaweza kuwa na athari mbaya.

XS
SM
MD
LG