Takwimu za Jumatano kutoka idara ya taifa ya takwimu zinaonyesha taifa hilo la pili lenye uchumi mkubwa sana duniani ukuaji wake ulikuwa kwa asilimia 4.9 kati ya Julai na Septemba ikilinganishwa na kipindi sawa na hicho mwaka uliopita.
Ongezeko hilo ni bora kuliko lililokisiwa na wachambuzi kadhaa la asilimia 4.5, lakini ni chini ya asilimia 6.3 iliyoshuhudiwa katika miezi mitatu iliyopita. Takwimu hizo pia zimeonyesha kuwa mapato ya ndani ya nchi yaliongezeka kwa asilimia 1.3 kwenye robo ya 3 ya mwaka, ikilinganishwa na 0.8 katika kipindi kati ya Aprili na Juni mwaka huu.
Sekta ya viwanda na madini iliimarika kwa asilimia 4.5 mwezi uliopita kipindi sawa na hicho mwaka uliopita, wakati sekta ya uuzaji ikikuwa kwa asilimia 5.5 mwezi uliopita kulinganishwa na wakati kama huo mwaka uliopita. Ukuaji wa China uliotarajiwa baada ya kuondolewa kwa kanuni za kuzuia maambukizi ya Covid-19 mwaka jana, bado haujapatikana
Forum