Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Oktoba 30, 2020 Local time: 08:17

Uchaguzi Zimbabwe wagubikwa na dosari


Mpiga kura katika kituo cha Mbare,Harare, July 31, 2013.
Mamilioni ya Wazimbabwe wamepiga kura leo Jumatano katika hali ya wasiwasi ambapo rais wa muda mrefu Robert Mugabe na waziri mkuu Morgan Tsvangirai wanagombania kiti cha rais.Na mara baada ya vituo vya kupigia kura kufunguliwa, upinzani ulianza kulalamika juu ya dosari kwenye zoezi hilo.

Katika muda wa saa mbili tu baada ya vituo vya kupigia kura kufunguliwa chama cha Movement for Democratic Change (MDC) kilianza kumshtumu rais Mugabe na chama chake cha ZANU-PF kwa dosari chungu nzima ikiwemo kuingilia kati orodha ya wapiga kura waliosajiliwa, kuwatishia wafuasi wa upinzani na hata kuwakamata wanaharakati. Makundi ya kutetea haki za binadamu pia yametoa malalamiko sawa na upinzani.

Tsvangirai anagombani urais kwa mara ya tatu wakati Mugabe anagombania kwa mara ya tano. Na katika umri wa miaka 89, ni kiongozi mkongwe zaidi duniani. Ametwala Zimbabwe tangu ilipopata uhuru wake mwaka wa 1980.

Kwa mujibu wa katiba mpya ya Zimbabwe rais anatakiwa kuhudumu kwa mihula miwili ya miaka mitano kila mmoja. Jana jioni Mugabe aliwaambia waandishi habari kuwa ataondoka madarakani endapo atashindwa lakini akaongeza kuwa haoni dalili zozote za kushindwa katika uchaguzi huu.

Tume ya uchaguzi nchini humo ina hadi Agosti 5 kutangaza matokeo.
Matokeo ya uchaguzi

Kura ya Maoni : Uchaguzi Tanzania

Kama unapiga kura leo utampigia nani kura yako ya urais?

Kura hii ya maoni si ya kisayansi na inaonyesha maoni ya waliojibu maswali tu.

Kama unapiga kura leo utampigia nani kura yako ya urais?

Kura hii ya maoni si ya kisayansi na inaonyesha maoni ya waliojibu maswali tu.

XS
SM
MD
LG