Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 01, 2023 Local time: 11:53

Uchaguzi wa magavana Nigeria wagubikwa na ghasia.


Wananchi wa Nigeria wakijiandikisha kupiga kura kabla siku ya uchaguzi wa magavana Jumanne Aprili 26.

Raia wa Nigeria wanapiga kura kuchagua magavana katika uchaguzi wa mwisho kabisa kote nchini ambao tayari umegubikwa na vurugu na ghasia.

Raia wa Nigeria wanapiga kura kuchagua magavana katika uchaguzi wa mwisho kabisa kote nchini ambao tayari umegubikwa na vurugu na ghasia. Mabomu matatu yalipiga kaskazinimashariki mwa mji wa Maiduguri jumanne, siku mbili baada ya milipuko katika mji huohuo kuuwa watu watatu na kujeruhi wengine 14.

Polisi imesema hakuna majeruhi katika milipuko ya mabomu hiyo mipya

Vituo vya kupigia kura vilifunguliwa kote nchini Jumanne huku kukiwa na mamia ya wafanyakazi katika uchaguzi. Kundi la kutetea haki za binadamu nchini Nigeria linasema karibu watu 500 wamekufa ktika ghasia za baada ya uchaguzi uliomwingiza madarakani rais Goodluck Jonathan.

Waislamu wanaomuunga mkono mgombea urais aliyeshindwa Muhammadu Buhari walivamia makanisa, nyumba, na vituo vya polisi hivyo kuchochea ghasia za kujibu mashambulizi kutoka kwa wakristo.

Buhari anasema uchaguzi uliibiwa na ameapa kupinga matokeo hayo mahakamani.

XS
SM
MD
LG