Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Julai 21, 2024 Local time: 20:37

Mchumi wa benki ya dunia asuasua uchaguzi wa Peru


Pedro Pablo Kuczynski
Pedro Pablo Kuczynski

Mchumi wa zamani wa Benki Kuu ya Dunia mwenye umri wa miaka 77 anaongoza kwa kura chache dhidi ya mtoto wa rais wa zamani wa Peru, Alberto Fujimori, katika duru ya pili ya uchaguzi wa rais nchini humo.

Huku ikiwa kura zaidi kidogo ya nusu zilizohesabiwa Jumatatu, Pedro Kuczynski ana asilimia 50.6 ya kura dhidi ya Keiko Fujimori mwenye asilimia 49.4.

Kuczynski amesema. “Wataunda na serikali kutokana na maridhiano." Akisema "hakuna tena haja ya kugombana tena."

Keiko Fujimori aliwaasa wapiga kura wake kusubiri kwa hamu. "Tutasubiri kwa makini kwa sababu kura za usiku kucha zitaingia kutoka majimboni na nje ya nchi na kutoka kwa wapiga kura wa vijijini" aliongeza.

XS
SM
MD
LG