Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 04, 2023 Local time: 16:17

Uchaguzi wa Mali


Mwanamke akipiga kura katika duru ya pili ya uchaguzi Bamako, Mali, August 11, 2013.
Mwanamke akipiga kura katika duru ya pili ya uchaguzi Bamako, Mali, August 11, 2013.
Wananchi wa Mali wamepiga kura Jumapili kumchagua rais ambaye wengi wanategemea ataondoa taifa hilo kwenye lindi la msukosuko wa kisiasa uliodumu kwa miezi 18.

Waziri mkuu wa zamani Ibrahim Boubacar Keita anapambana na waziri wa zamani wa fedha Soumalia Cisse katika uchaguzi huo wa marudio ambao wachambuzi wanasema utaleta mwelekeo mpya kwa taifa hilo la Afrika Magharibi.

Katika duru ya kwanza ya uchaguzi hapo Julai 28, Keita alipata takriban asili mia 40 ya kura huku Cisse akipata asili mia 20. Wagombea urais wengine miongoni mwa 25 ambao walioondolewa katika duru ya kwanza wamesema wanamuunga mkono bw. Keita akiwemo Dramane Dembele ambaye alipata nafasi ya tatu katika duru ya kwanza ya uchaguzi huo.

Huu ni uchaguzi wa kwanza tangu mwaka wa 2007 ambao huenda ukafungua milango ya msaada wa dola bilioni 4 zilizoahidiwa na jamii ya kimataifa, lakini ukasimamishwa baada ya mapinduzi ya serikali yaliyofanywa na majeshi na kutumbukiza taifa hilo katika machafuko.
XS
SM
MD
LG