Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Februari 11, 2025 Local time: 06:13

Uchaguzi wa Mali wa mwakani wasogezwa mbele tena


Serikali ya kijeshi ya Mali, imeahirisha uchaguzi wa rais ambao ulitarajiwa kurudisha taifa hilo la Afrika magharibi kwenye demokrasia kufuatia mapinduzi ya 2020, msemaji wa serikali amesema Jumatatu.

Uchaguzi wa rais uliopangwa kufanyika Febuari 2024, umeahirishwa kwa sababu za kiufundi ili kuruhusu serikali ya mpito kupitia taarifa za uchaguzi, kuruhusu vifungu vipya vya katiba ambavvyo vitachelewesha duru ya pili ya uchaguzi, amesema msemaji wa serekali Abdoulaye Maiga alipozungumza na wanahabari katika mji mkuu wa nchi hiyo, Bamako.

Ni mara ya pili kwa serekali ya kimapinduzi ya Mali ambayo imetokana na mapinduzi mawili mwaka 2020 kuahirisha uchaguzi wa rais wa nchi.

Wanasiasa wa Mali wamekosoa uamuzi huo ambao unaweza kusababisha vikwazo vya kiuchumi kwa Mali kutoka jumuiya ya mataifa ya magharibi ECOWAS.

Jumuiya hiyo ililegeza vikwazo kwa Mali Julai 2022 baada ya serikali kuahidi kufanya uchaguzi.

Forum

XS
SM
MD
LG