Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Februari 26, 2024 Local time: 10:45

Uchaguzi wa Malawi wabatilishwa


Rais wa Malawi Joyce Banda
Rais wa Malawi Joyce Banda

Vyombo vya habari vimemnukulu mkuu wa tume ya uchaguzi Maxon Mbendera akisema kuwa mchakato wa kuhesabu kura utaendelea na kwamba rais hana mamlaka ya kubatilisha uchaguzi rasmi.

Rais wa Malawi Joyce Banda amebatilisha uchaguzi wa urais uliofanywa wiki hii kutokana na kasoro za masanduku ya kura, lakini maafisa wa uchaguzi mara moja wakapinga maamuzi yake.

Akizungumza na waandishi habari Jumamosi, rais Banda alisema ana mamlaka kikatiba kubatilisha kura hiyo na kuelezea kwamba matukio kadhaa ikiwemo uingiliaji kati wa masanduku ya kura na kuongezewa kwa masanduku ya kura yasiyo halali kumesababisha achukue hatua hiyo.

Bi Banda pia amesema uchaguzi mwingine utafanyika ndani ya siku 90, na kwamba yeye hatagombea urais.

Alisema alitumaini kushinda uchaguzi huo na kuongoza Malawi kwa muhula mwingine, baada ya kuliongoza taifa hilo kwa miaka miwili kufuatia kifo cha mtangulizi wake Bingu wa Mutharika.

Vyombo vya habari vimemnukulu mkuu wa tume ya uchaguzi Maxon Mbendera akisema kuwa mchakato wa kuhesabu kura utaendelea kufuatia uchaguzi wa Jumanne wiki hii na kwamba rais hana mamlaka ya kubatilisha uchaguzi rasmi.
XS
SM
MD
LG