Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Juni 18, 2024 Local time: 15:36

Uchaguzi wa awali kuwania urais wafikia hatua muhimu


Mgombea wa urais wa Republican, Donald Trump.
Mgombea wa urais wa Republican, Donald Trump.

Vituo vya kupigia kura vimefunguliwa leo katika jimbo la Indiana, mahali ambapo mgombea wa urais wa Republican anayeongoza, Donald Trump, anakabiliwa na wakati mgumu kwenye uchaguzi huu wa awali na mpinzani wake wa karibu, Seneta wa Texas, Ted Cruz.

Ushindi wa Trump katika jimbo la Indiana utamuweka kwenye njia kuelekea uteuzi wa urais kwa chama cha Republican kabla ya mkutano mkuu wa unaotarajiwa kufanyika huko Cleveland mwezi Julai.

Ukusanyaji maoni wa hivi karibuni uliofanywa na kituo cha televisheni cha NBC News, Wall Street Journal na Marist unampa Trump uongozi kwa point 15 huko Indiana, japokuwa mbali mbali za awali zinatofautiana kuhusu kiwango chake cha ushindi.

XS
SM
MD
LG