Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 07:54

Waghana wanajiandaa kupiga kura wakiwa na wagombea wakuu wanaofahamika


Wagombea urais wa Ghana rais wa sasa Nana Akufo Addo kushoto na mpinzani wake rais wa zamani na mtangulizi wake John Dramani Mahama.
Wagombea urais wa Ghana rais wa sasa Nana Akufo Addo kushoto na mpinzani wake rais wa zamani na mtangulizi wake John Dramani Mahama.

Waghana wanaenda kupiga kura Jumatatu huku Rais wa sasa Nana Akufo-Addo na rais wa zamani John Mahama wakiwa wagombea wa juu. Chama cha Akufo-Addo kimefanya kampeni kikinadi juu ya mipango yake ya elimu, wakati cha Mahama kimejikita katika kufungua nafasi za ajira na kushambulia rekodi ya mpinzani wake juu ya ufisadi.

Serikali ya Ghana wiki hii ilitangaza kuwa Jumatatu, Desemba 7, itakuwa ni siku ya mapumziko ili kupata wapiga kura wengi zaidi kumchagua rais ajaye. Licha ya zaidi ya wapiga kura milioni 17 waliojiandikisha na wagombea urais 12, mamlaka zinapambana juu ya kutafuta huruma ya wapiga kura huku kukiwa na wagombea wa juu wanaojulikana kutoka katika chaguzi mbili zilizopita.

Rais wa sasa anakabiliana na mtangulizi wake rais wa zamani

Rais wa sasa Nana Akufo-Addo wa New Patriotic Party (NPP) anakabiliana dhidi ya mtangulizi wake, John Mahama wa chama cha upinzani cha National Democratic Congress (NDC). Mahama alishinda katika uchaguzi wa 2012 na kisha akashindwa na Akufo-Addo katika uchaguzi wa 2016.

Kojo Asante wa Kituo cha Maendeleo ya Kidemokrasia cha Ghana. Anasema kuna kuchoshwa na hali ya juu haswa kati ya tabaka la kati

“Saa chache za kwanza daima ni kiashiria kizuri ikiwa watu watatoka nje. Ikiwa wataona umati wa watu na wanajiheshimu na kisha kupata maoni kwamba ni rahisi sana kwenda kupiga kura , hatimaye huenda watakwenda, hata ikiwa mwanzo hawakutaka kufanya hivyo.”alisema.

Licha ya changamoto hiyo, Asante anasema uchunguzi wao kabla ya uchaguzi unaonyesha Waghana wana wasiwasi juu ya maswala kama vile kuboresha miundombinu na ajira.

Utafiti huo ulionyesha majibu mazuri juu ya maamuzi ya NPP ya kupambana na COVID-19, vifaa vya umeme, na elimu.

Lakini umma haukuvutiwa sana na rekodi ya Akufo-Addo juu ya mfumuko wa bei, ukosefu wa usawa, na ufisadi.

Kumshambulia Akufo-Addo juu ya ufisadi ilikuwa lengo la kampeni ya Mahama, pamoja na kufungua nafasi za ajira.

Lakini mtalaam wa taaisis ya ushauri ya Songhai Khobi Annan anasema viongozi wote hawa wamefanya vibaya madarakani.

“Ni chaguo gumu kwa watu wengi. Hakuna hata mmoja wao aliyefanya kazi nzuri wakati akiwa madarakani, na nadhani itabakia katika mambo ya kimsingi kama vile elimu, ufisadi,na utengenezaji wa ajira. “ alisema akiongeza “nadhani utengenezaji wa ajira na elimu haswa ndio yanaathiri watu wengi kila siku kuliko ufisadi.”

Chini ya urais wa Mahama, kulikuwa na shida ya nishati, kashfa za ufisadi na kushuka kwa thamani ya fedha. Mnamo mwaka wa 2016, NPP ilishinda kwa kura kama milioni moja na kwa matarajio makubwa kwa Akufo-Addo kumaliza ufisadi.

Lakini katika wiki kadhaa kabla ya uchaguzi wa mwaka huu, chama cha upinzani cha NDC kilitoa madai ya ufisadi dhidi ya Akufo-Addo. Mwendesha mashtaka maalum wa kupambana na ufisadi wa Ghana alijiuzulu wiki tatu tu kabla ya uchaguzi, akidai kuingiliwa kisiasa.

Wakati Akufo-Addo akikana ufisadi wowote katika utawala wake, wachambuzi wanasema ni ngumu kujua ikiwa madai hayo yataathiri kura hiyo.

Bila kujali matokeo, au idadi ya wapiga kura, wachambuzi wanatarajia uchaguzi wa Ghana utakuwa wa haki na amani kama na chaguzi mbili zilizopita.Chuo Kikuu cha Ghana kilichapisha utafiti wa wapiga kura ambao uliipa NPP makadirio ya kuongoza kwa asilimia 11 juu ya NDC na asilimia tano ya wapiga kura wakiwa hawajaamua.

Imetayarishwa na Sunday Shomari,VOA,Washington DC

XS
SM
MD
LG