Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Julai 17, 2024 Local time: 20:14

Uchaguzi mdogo Tanzania wakumbwa na upinzani mkali


Uchaguzi wa serikali za mitaa huko Tanzania unaelezewa kugubikwa na kasoro nyingi za kiutendaji
Uchaguzi wa serikali za mitaa huko Tanzania unaelezewa kugubikwa na kasoro nyingi za kiutendaji

Mchuano wa matokeo ya uchaguzi wa serilkali za mitaa nchini Tanzania uliofanyika jumapili baina ya chama tawala CCM na vile vya upinzani umekuwa na upinzani mkali.
Wakati matokeo hayo yakiendelea kutolewa takwimu zinaonyesha kwamba licha ya CCM kufanya vyema kwenye maeneo mengi lakini hata hivyo imezidiwa nguvu kiasi na chama cha upinzani cha Chadema ambacho pia ni sehemu ya muungano wa vyama vinavyounda umoja wa UKAWA.

please wait

No media source currently available

0:00 0:02:58 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Mchuano huo umejitokeza katika maeneo yanayojatwa kuwa na mwamko mpya wa kisiasa ikiwemo mkoa wa Dar Es Salaam ambapo ripoti zinaonyesha kuwa vyama hivyo viwili vimekuwa vikichuana vikali.

Baadhi ya wananchi wakielezea hisia zao kabla ya uchaguzi mdogo kufanyika
Baadhi ya wananchi wakielezea hisia zao kabla ya uchaguzi mdogo kufanyika

Kwa ujumla uchaguzi huo ambao umekumbwa na dosari za hapa na pale kiasi cha kusababisha baadhi ya maeneo kuahirisha kufanya harakati zake za siku unafuatiliwa na wengi kwa vile matokeo yake yanategemea kutoa mwelekeo halisi kuhusiana na uchaguzi mkuu wa mwakani.

Kumekuwana shutuma kila upande ukilalamikia kutowajibika ipasavyo kiasi cha kusabisha vurugu na kuvuruga zoezi la upigaji wa kura.

Hali ya kutoelewana ilijitokeza katika maemeo kadhaa ikiwamo eneo la Mwenge na kusabisha askari polisi kurusha hewani risasi ili kutawanya wapiga kura.

Akizungumzia kuhusu hali ilivyojitokeza kwenye uchaguzi huo, Makamu Katibu Mkuu wa Chadema bara, bwana John Mnyika amewaambia waandishi wa habari jumatatu kuwa chama hicho kimevunjwa moyo na namna kasoro zilizojitokeza kwenye zoezi la upigaji kura.

Naye waziri anayehusika na tawala za mikoa na serikali za mitaa bibi. Hawa Ghasia alielekeza lawama kwa kambi ya upinzani akisema kuwa upande huo ndiyo uliohusika kwenye kuvuruga zoezi hilo.

Wakati huo huo Sauti ya Amerika-VOA ilizungumza na Harold Sungusia wa kituo cha sheria na haki za binadamu nchini Tanzania ambaye alikuwa akiangalia uchaguzi huu na yafuatayo ni maelezo yake.

please wait

No media source currently available

0:00 0:03:01 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Uchaguzi huo unafanyika huku wananchi wakiendelea kutupa lawama zao kwa serikali kuu ambayo inalaumiwa kwa kuchelewa kutoa maamuzi kuhusiana na kashfa ya uchotaji wa fedha katika akaunti ya ESCRO.

XS
SM
MD
LG