Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Februari 25, 2024 Local time: 11:01

Raia wa Burundi wapiga kura

Mgombea pekee wa uchaguzi wa urais Burundi, Rais aliyeko madarakani Pierre Nkurunziza akiwapungia wafuasi wake mikono wakati wa kampeni huko Rugombo Mei 14 mwaka huu.
Mgombea pekee wa uchaguzi wa urais Burundi, Rais aliyeko madarakani Pierre Nkurunziza akiwapungia wafuasi wake mikono wakati wa kampeni huko Rugombo Mei 14 mwaka huu.

Vituo vya uchaguzi nchini Burundi vimeshafungwa, katika uchaguzi wa rais wenye mgombea mmoja tu kufuatia kampeni za uchaguzi kugubikwa na mashambulizi ya gruneti ambayo yaliuwa watu wasiopungua watano.

Rais aliyeko madarakani Pierre Nkurunziza, hana mpinzani katika uchaguzi huo wa Jumatatu, baada ya upinzani kujitoa katika kinyang’anyiro hicho kwa shutuma za kuzagaa kwa wizi.

Mivutano bado ipo juu nchini humo ambapo zaidi ya magruneti matatu yalilipuka usiku wa kuamkia Jumatatu, ikiwemo shambulizi moja karibu na ofisi za kazi za wafuatiliaji uchaguzi kutoka Umoja wa Ulaya.Hakuna majeruhi walioripotiwa katika milipuko yeyote. Polisi wanasema wanaungana na jeshi kulinda sheria na hali inadhibitiwa.

Huku kukiwa wazi mshindi atakuwa nani watu wachache waliripotiwa kujitokeza katika upigaji kura ikilinganishwa na uchaguzi mdogo uliofanyika nchini humo mwezi uliopita. Wale ambao walijitokeza walipewa makaratasi ya kupiga kura na bahasha mbili, bahasha moja nyeupe kwa ajili ya kumuunga mkono bwana Nkurunziza na bahasha nyeusi kwa ajili ya kumpinga bwana Nkurunziza.

Uchaguzi wa Jumatatu ni wa kwanza kufanyika tangu kutiwa saini mkataba wa amani mwaka 2005 uliomaliza miaka 13 ya vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Raia wa Burundi watapiga kura tena mwezi Julai katika duru ya pili ya uchaguzi wa wabunge ikifuatiwa na uchaguzi wa tarafa mwezi Septemba.

XS
SM
MD
LG