Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Aprili 17, 2024 Local time: 02:32
VOA Direct Packages

Uchafu wa plastiki kwenye bahari waongezeka kwa viwango vya kutisha


Picha ya eneo la kutupia taka za plastiki
Picha ya eneo la kutupia taka za plastiki

Ripoti kutokana na utafiti ulioongozwa na shirika la 5 Gyres la Marekani linaloongoza kampeni ya kupunguza uchafu wa plastiki limesema Jumatano kwamba viwango vya plastiki vinavyoingia baharini tangu 2005 ni vingi mno.

Ripoti zinaendelea kusema kwamba viwango huenda vikaongezeka mara nne kufikia 2040, iwapo hatua za haraka hazitachukuliwa. Kulingana na ripoti hiyo, takriban chembechembe trilioni 171 za plastiki zilikuwa baharini kufikia 2019.

Utafiti huo ulikusanya data za uchafu wa plastiki kwenye maji ya bahari kutoka vituo 11,777, na kwenye maeneo 6 muhimu ya bahari kuanzia 1979 hadi 2019. Marcus Eriksen ambaye ni mwanzilishi mwenza wa 5 Gyres amesema kwamba kunahitajika mkataba wenye nguvu kutoka kwa Umoja wa Mataifa unaositisha uchafuzi wa plastiki kote ulimwenguni kwa kudhibiti vyanzo vyake.

Wataalam wamesema kwamba ripoti hiyo imefichua kwamba tatizo la uchafuzi wa plastiki kwenye bahari halijapewa uzito unaohitajika.

XS
SM
MD
LG