Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Aprili 24, 2024 Local time: 11:11

Washukiwa wawili wa uhalifu wasakwa Ubelgiji


Askari polisi akiwa analinda jengo ambalo lilitumika na polisi wakati wa msako wao
Askari polisi akiwa analinda jengo ambalo lilitumika na polisi wakati wa msako wao

Maafisa wamesema mshukiwa mmoja ambaye aliuwawa wakati wa shambulizi alikuwa raia wa Algeria aliyezaliwa mwaka 1980, akiwa na angalau rekodi moja ya wizi.

Waendesha mashtaka wa serikali kuu ya Ubelgiji wanasema washukiwa wawili bado hawajapatikana baada ya shambulizi lililofanywa na polisi kwenye nyumba ya kupangisha katika viunga vya Brussels hapo jana.

Katika mkutano na waandishi wa habari hii leo, maafisa wamesema mshukiwa mmoja ambaye aliuwawa wakati wa shambulizi alikuwa raia wa Algeria aliyezaliwa mwaka 1980, akiwa na angalau rekodi moja ya wizi.

Raia watatu wa Ubelgiji na ofisa polisi mmoja wa Ufaransa walijeruhiwa wakati wa operesheni hiyo ya pamoja ya mataifa mawili, pale risasi zilizpoanza kufyetuliwa katika viunga vya Forest.

XS
SM
MD
LG