Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 06:16

Ubalozi wa Marekani waidhinisha kuondoka kwa hiari kwa wafanyakazi wake na familia Ethiopia


Msafra wa magari ya umoja wa mataifa ukirudishwa na wanajeshi wa Ethiopia karibu na Agula katika jimbo la Tigray kutokna na mapigano.
Msafra wa magari ya umoja wa mataifa ukirudishwa na wanajeshi wa Ethiopia karibu na Agula katika jimbo la Tigray kutokna na mapigano.

Ubalozi wa Marekani mjini Addis Ababa umeidhinisha kuondoka kwa hiari kwa baadhi ya wafanyakazi wake na familia zao huku wapiganaji wa kundi la TPLF kutoka kaskazini mwa Ethiopia wakipiga hatua kuelekea mji mkuu.

Uamuzi huo umetolewa baada ya Marekani kusema Jumatano "ina wasiwasi mkubwa" kuhusu uhasama unaoenea na kutaka kusitishwa kwa operesheni za kijeshi ili kuunga mkono mazungumzo ya kusitisha mapigano.

Serikali ya Waziri Mkuu Abiy Ahmed imetangaza hali ya hatari, huku wanajeshi kutoka jimbo la kaskazini la Tigray wakitishia kusonga mbele hadi Addis Ababa.

msemaji wa chama cha Tigray People's Liberation Front (TPLF), Getachew Reda, alisema Jumatano jioni kwamba Wapiganaji wao wako katika mji wa Kemise katika jimbo la Amhara, kilomita 325 kutoka mji mkuu,.

Ubalozi wa Marekani umesema katika taarifa yake kwamba kuna uwezekano wa kuongezeka ghasia zaidi na si salama kusafiri kwenda Ethiopia.

"Wizara ya mambo ya nje iliidhinisha kuondoka kwa hiari kwa wafanyakazi wa serikali ya Marekani wasio wa dharura na wanafamilia wa wafanyakazi hao kutoka Ethiopia kutokana na vita vya silaha, machafuko ya wenyewe kwa wenyewe, na uwezekano wa uhaba wa usambazaji," ilisema.

Serikali hapo awali ilizuia au kuzima huduma za intaneti na simu wakati wa machafuko iliongeza.

XS
SM
MD
LG