Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Julai 18, 2024 Local time: 15:15

Tyler Perry awachangia watoto Albino kutoka Tanzania


Watoto wenye ulemavu wa ngozi yaani Albino kutoka nchini tanzania.
Watoto wenye ulemavu wa ngozi yaani Albino kutoka nchini tanzania.

Mtengenezaji filamu nchini Marekani, Tyler Perry alitoa mchango wa takriban dola 200,000 kusaidia ujenzi wa nyumba kwa watoto wa kitanzania wenye ulemavu wa ngozi yaani Albino ambao walikatwa baadhi ya viungo vyao vya mwili.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Associated Press-AP, msemaji wa Perry, Kaleigh Thomas alisema Jumatatu kuwa mtengenezaji filamu huyo alisaidia ujenzi wa nyumba ya vyumba vinne katika jimbo la New Jersey nchini Marekani. Alisema watoto hao watakaa huko huku wakipatiwa matibabu nchini Marekani.

Perry alitoa mchango huo baada ya kuangalia makala maalumu ikimuelezea Elissa Montanti, mwanamke kutoka Staten Island ambaye anaendesha shirika moja lisilo la kiserikali la Global Medical Relief Fund linalowasaidia watoto walioathiriwa na vita pamoja na majanga ya asili.

Montanti hivi karibuni aliwaleta nchini Marekani watoto wenye ulemavu wa ngozi kutoka Tanzania. Watoto hao walikatwa viungo katika mashambulizi. Sehemu za viungo vyao viliuzwa kwa imani kwamba watoto wenye ulemavu wana nguvu za kipekee za kuleta utajiri na bahati.

XS
SM
MD
LG