Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 22, 2024 Local time: 08:02

Mo Ibrahim Ashindwa Kumpata Mshindi wa Tuzo ya Uongozi Afrika


Mo Ibrahim
Mo Ibrahim

Tajiri mkubwa na mashuhuri wa biashara ya mawasiliano wa Sudan, Mo Ibrahim ameshindwa kumpata mshindi wa tuzo ya dola milioni 5 ambayo hutolewa kwa kiongozi bora zaidi wa kisiasa barani Afrika, kwa mwaka wa pili mfululizo.

Tuzo hiyo inalengo la kuimarisha demokrasia lakini kwa kipindi hiki hakuna kiongozi aliyefikia sifa ya kunyakua tuzo hiyo.

Tangu kuzinduliwa mwaka wa 2006 ni viongozi wanne tu ambao wamepokea tuzo hiyo, ikiwa ni pamoja na Rais wa Mozambique Joaquim Chissano. Festus Mogae wa Botswana, De Verona Rodrigues Pires wa Cape Verde pamoja na Hifikepunye Pohamba wa Namibia.

Ili kiongozi apate tuzo hiyo, lazima awe alichaguliwa kidemokrasia, na awe ameachia madaraka miaka mitatu iliopita kwa mujibu wa muda uliowekwa na katiba.

Japokuwa watu wenye sifa za kuweza kupokea tuzo hii wanazidi kuwa wachache katika bara ambalo linalojulikana kwa mapinduzi na viongozi wanaonang'ania madarakani.

Tuzo hiyo humpatia mshindi jumla ya dola milioni 5 zinazotolewa kwa kipindi cha miaka kumi na malipo ya uzeeni ya dola laki mbili kila mwaka.

XS
SM
MD
LG