Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 17:20

Uturuki na Israel warejesha uhusiano wa kibalozi


Mawaziri wakuu wa Uturuki na Israel wametangaza kurudisha uhusiano kamili wa kidiuplomasia baina yao ambao ulisita kwa miaka 6 kufwatia kuuliwa kwa wanaharakati wa Uturuki waliotaka kuvunja kizuizi cha uchumi cha Israel katika ukanda wa Gaza.

Waziri mkuu wa Uturuki Binali Yidirim alitangaza kuwa mataifa hayo mawili yatawarudisha mabalozi wao haraka iwezekanavyo. Kurudishwa kwa uhusiano kamili wa kidiplomasia kunafwatia takriban mwaka mzima wa majadiliano ya siri.

Uhusiano ulivurugika pale makomandoo wa Israel walipo wauwa wanaharakati 10 wa uturuki walojaribu kuingia kwa kutumia meli huko Gaza, ambayo ilikuwa imewekewa kizuizi cha bahari mwaka 2010.

Kulingana na makubaliano hayo, Bw. Yildirim alisema, Israel itawalipa familia za wanaharakati walouwawa fidia ya dola millioni 20.

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, akizungumza huko Rome, alisema kizuizi cha bahari cha Gaza kitaendelea, akisema ni muhimu kwa kuzuia kuingizwa kwa silaha. Ankara imekuwa ikidai Israel kunyanyuwa vikwazo kabla kurudisha uhusiano kamili wa kibalozi.

Yildirim alisema, kwa mujib wa makubaliano, Uturuki itakubaliwa kupeleka misaada Gaza kupitia Israel.

Anasema meli ya kwanza itajaza zaidi ya tani elfu 10 ya misaada ya kibinadam itaondoka kuelekea mji wa bandari wa Ashdod huko Israel ijumaa.

Yildirim anasema kulingana na makubaliano, kizuizi cha Israel kitakuwa kimemalizika. Anasema pia kuwa uturuki itajenga hospitali yenye vitanda mia 2 huko Gaza.

Mshauri wa kisiasa mwenye makao yake Istanbul, Atilla Yesilada kutoka shirika la Global Source Partners, anasema maslahi ya pamoja ndio yanayosukuma makubaliano hayo.

Yesilida alisema, kuna sababu za kisiasa kadhalika sababu za kiuchumi, bila shaka suala la vita Syria vimeshawishi wote Israel na Uturuki kufanya maridhiano. Israel ilikuwa ikihofu mpaka wake na Syria unaweza kudhibitiwa na makundi yenye siasa kali.

Israel na Uturuki awali walikuwa na uhusiano wa karibu wa hata uhusiano wa kijeshi.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry alikaribisha hatua hiyo. Washington imekuwa ikipigania kurejeshwa kwa uhusiano wa kidiplomasia baina ya mataifa hayo mawili muhimu ambyo ni washirika wake.

Wafatiliaji wanasema licha ya mivutano ya hivi karibuni, biashara baina ya pande hizo mbili zimekuwa zikiendelea. Netanyahu anasema makubaliano hayo yatakuwa na athari kubwa kiuchumi kwa Israel.

XS
SM
MD
LG