Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 16:50

Uturuki kurejesha uhusiano na Misri


Rais wa Uturuki, Tayyip Erdogan Erdogan.
Rais wa Uturuki, Tayyip Erdogan Erdogan.

Ankara ilikata uhusiano wa kidplomasia na Cairo baada ya kupinduliwa kwa rais wa zamani wa Misri, Mohammed Morsi.

Kuna ishara kuwa washirika wa zamani Uturuki na Misri wamechukuwa hatuwa za kwanza za kurudisha uhusiano. Ankara ilikata uhusiano wa kidplomasia na Cairo baada ya kupinduliwa kwa rais wa zamani wa Misri, Mohammed Morsi.

Wiki hii, Ankara ilikaribisha kuhusika kwa Cairo kwenye kundi la kimataifa la kutatuwa mzozo wa Libya.

Hatua hiyo ilifwatia ripoti kuwa rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan kuruhusu kurudishwa uhusiano na Misri katika kiwango cha uwaziri. Uhusiano wa kidiplomasia ulikatwa baada ya jeshi la Misri kumpinduwa rais Mohammed Morsi, ambaye alikuwa mshirika wa karibu wa Bw. Erdogan.

Mwandishi wa masuala ya kisiasa Semih Idiz wa gazeti la Cumhuriyet, na mtandao wa Al Monitor, anasema hatua ya kurudisha uhusiano na Misri na mataifa mengine ya Mashariki ya kati, inafwatia kudhoofika kwa uhusiano wa Uturuki na majirani zake wa kusini pamoja na Russia.

Idiz alisema, Uturuki imejikuta imetengwa huko Mashariki ya kati, na inalazimika kujaribu kurudisha baadhi ya uhusiano uliokuwa na mataifa hayo hapo awali.”

Uhusiano wa Ankara na Saudi Arabia, umeboreka tangu kuingia madarakani mfalme mpya, Salman . Mataifa hayo mawili yanaratibu kwa karibu msaada wao kwa waasi wa Syria.

Mtaalam wa uhusiano wa kimataifa, Soli Ozel, kutoka chuo kikuu cha Kadir mjini Istanbul, anasema hatua za Uturrki kurudisha uhusiano na Misri zinatokana na kuboreka kwa uhusiano wa Uturuki na Saudi Arabia.

Ozel anasema, Uturuki haiwezi kuzidisha uhusiano na Saudi Arabia na huku wakiwa na uhusiano mdogo tu na Misri, ambayo inadhaminiwa na Saudi Arabia. Anasema, kumbuka adui wa pamoja wa mataifa haya matatu ni Iran.

Uturuki, Saudi Arabia na Misri wote wana wasiwasi na nguvu za Iran katika kanda hiyo itakuwa, kwa vile sasa vikwazo vya kimataifa dhidi yake vimeondolewa. Viongozi hao watatu watakuwa na nafasi ya kukutana ana kwa ana katika mkutano ujao wa kiislamu, unaotarajiwa kufanyika mjini Istanbul mwezi Aprili.

Bw Idiz anasema Erdogan anafaamu kuwa wazo la kurudisha uhusiano na Misri in suala tete ndani ya chama chake cha AKP, kutokana na jinsi serikali ya Misri ilivyowatendea wafuasi wa kundi la Muslim Brotherhood.

Hata hivyo, msimamo mgumu wa Cairo unaonekana kutatiza suala zima, kutokana na uungaji mkono wa dhati wa Ankara, kwa serikali ya Hamas huko Gaza.

Bw Ozel anasema, hatima ya rais wa zamani Morsi ambaye anakabiliwa na hukumu ya kifo ndio sula muhimu. Anasema iwapo Misri itamnyonga Morsi, basi anadhani , itakuwa vigumu kuendeleza uhusianohuo ulofufuliwa.

Wachambuzi wanasema Erdogan anasukuma kufutwa kwa hukumu za vifo dhidi ya Bw. Morsi na wafuasi wake, na kuwepo uwezekano wa kuwapatia msamaha kamili, kama gharama kwa Misri kurudisha uhusiano kamili wa kidiplomasia na Uturuki.

XS
SM
MD
LG