Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Oktoba 04, 2022 Local time: 05:46

Tunisia: Zaidi ya vijana wadogo 2,000 waliondoka nchini mwao na kuelekea Italy


Kundi la wahamiaji wanaoaminika kuwa wahamiaji kutoka Tunisia wakiwa kwenye boti ya mbao wakisubiri kusaidiwa na timu ya shirika la hisani la Uispania, karibu na kisiwa cha Italy cha Lampedusa, Julai 29, 2021. Picha ya AP

Zaidi ya vijana wadogo 2,000 wa Tunisia walivuka bahari ya Mediterania mwaka huu kutoka katika taifa lao la kaskazini mwa Afrika kuelekea Italy kutafuta maisha bora, shirika la kutetea haki za binadamu limesema Jumatano.

Jukwaa la Tunisia la haki za kiuchumi na kijamii (FTDES) limesema watoto wadogo ni miongoni mwa jumla ya wahamiaji 10,139 wa Tunisia ambao walipita kwenye bahari ya Mediterania kuelekea Italy tangu mwanzoni mwa mwaka 2022.

Zaidi ya wahamiaji 14,700, wakiwemo wengi kutoka mataifa ya Kusini mwa Jangwa la Sahara, walizuiliwa na kurejeshwa nyuma katika kipindi hicho, FTDES imesema.

Umaskini unaochochewa na mzozo mbaya wa kiuchumi na kijamii unafanya hatari za bahari kuwa sababu ya pili kwa wahamiaji hao ambao wana ndoto ya maisha bora kwao wenyewe na watoto wao,” FTDES imesema.

Imekemea pia “siasa zisizo za kibinadamu za Umoja wa Ulaya, ambazo zinazuia uhuru wa kutembea wa wahamiaji.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG