Mahakama ya Tunisia siku ya Jumatano iliwahukumu waandishi wawili wa habari kifungo cha mwaka mmoja jela kwa tuhuma za kuchapisha habari za uongo zinazodhuru usalama wa umma, afisa mmoja wa mahakama alisema, huku kukiwa na ongezeko la hofu ya ukandamizaji unaolenga sauti zote muhimu.
Mourad Zghidi na Borhan Bsaiss, wote waandishi wa habari wa radio ya IFM, waliwekwa kizuizini mwezi huu kutokana na maoni ya kisiasa waliyotoa kwenye radio.
Tunisia sasa imewafunga jela jumla ya waandishi sita wa habari, ikiwa ni pamoja na Zghidi na Bsaiss, huku darzeni wengine wakikabiliwa na mashtaka mahakamani, kulingana na kundi la waandishi wa habari, ambalo ni chama kikuu cha waandishi wa habari nchini humo.
Forum