Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Oktoba 04, 2023 Local time: 13:02

Profesa Jay Azungumza na VOA


Msani mashuhuri kutoka Tanzania Profesa Jay, anatoa wito kwa wasani wenzake kutumia ujuzi na vipaji vyao katika kuendeleza jamii.

Rapper mashuhuri wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla Joseph Haule au maarufu kwa jina la Profesa Jay aliwasili kwenye studio za sauti ya Amerika na kuzungumza nasi.

Mwanamuziki huyu wa Hip hop ya Tanzania ijulikanayo kama “Bongo Flava” hivi sasa yupo hapa Marekani kwa ziara ya kimuziki ambapo tayari ameshafanya maonyesho huko Texas na Washington DC.

Akifuatana na Dj wake hapa Marekani Richard na mapromota wake wa DC Mambo Jambo alizungumzia mambo mengi ikiwa ni pamoja na jinsi alivyopata majina mbali mbali na ubalozi wake wa Malaria No more halikadhalika mipango yake ijayo.

Profesa Jay ameshinda tuzo mbali mbali za muziki ikiwemo ya Kilimanjaro Music Award 2004, Wimbo bora 2006 Nikusaidieje, 2007 wimbo Sivyo ndivyo na 2009 mwandishi bora wa muziki. Mwaka 2008 alikuwamo katika orodha ya MTV kwa nyimbo bora ya Hip hop.

Fuatana nasi kwenye mahojiano yetu na Profesa Jay.

XS
SM
MD
LG